Dawa Mpya Ya Saratani Inayozuia Uvimbe Yawapatia Matumaini Wagonjwa

Dawa ya saratani
Dawa ya 'Berzosertib' inayoweza kuzuia seli za saratani kujikarabati zenyewe imeonesha ishara za mapema za kufanya kazi.
Zaidi ya nusu ya wagonjwa 40 wa saratani waliopewa dawa ya Berzosertib iliwasaidia kuzuia uvimbe mwilini.
''Berzosertib ina uwezo zaidi inapopewa mgonjwa ambaye tayari anafanyiwa tiba ya kemikali {chemotherapy}'', ulisema utafiti huo unaoendeshwa na taasisi ya saratani ICR na Royal Marsden.
Majaribio yalilenga kupima dawa hiyo.
Dawa hiyo ni ya kwanza kufanyiwa majaribio ambayo huzuia protini inayosaidia katika ukarabati huo wa seli. Inapoathirika Protini hiyo huzuia saratani kukarabati seli zake.
Ni miongoni mwa tawi la tiba kwa jina 'precision', ambazo hulenga jeni maalum ama mabadiliko ya jeni.
Utafiti huo ulishirikisha wagonjwa walio na uvimbe wa muda mrefu ambao hakuna dawa imefanikiwa kuwatibu.
Hiki ndicho kilichojulikana kama awamu ya kwanza ya majaribio, ambayo yametengenezwa kupima usalama wa tiba.
Lakini ICR imesema kwamba watafiti walipata ishara za mapema kwamba berzosertib inaweza kuzuia uvimbe kukuwa.


EmoticonEmoticon