Dawa ya Covid-19 Inayolenga Kukabiliana Na Kuganda Kwa Damu

Majaribio  Covid-19
Wanasayansi wanatarajiwa kufanya majaribio ya dawa kuona ikiwa inaweza kuzuia kuganda kwa damu kunakohusishwa na ugonjwa wa Covid-19.
Majaribio hayo, yaliyofadhiliwa na Wakfu wa British Heart yataangazia dhana ya kuwa mgando wa damu unasababishwa na kutosawazika kwa homoni kunakotonaka na maambukizi ya virusi vya corona.
Hiyo itakuwa moja ya dawa ambayo kwa sasa inafanyiwa majaribio ya kuzuia athari mbaya za ugonjwa wa Covid-29.
Theluthi moja ya wagonjwa waliolazwa kwasababu ya virusi vya corona, damu yao huganda na kuwaweka katika hatari zaidi.
Dawa hiyo ya TRV027, inafanya kazi ya kurekebisha homoni na kusiweka sawa zenye kuhusishwa na shinikizo la juu la damu, maji na chumvi
Wanasayansi wa chuo cha Imperial College London, wanaofanya majaribio hayo, wanafikiria kwamba virusi vinaingia ndani ya mwili, na kutumia kimeng'enya kama njia ya kuingia kwenye seli.
Lakini dawa hii inafanya kimeng'enya kutofanya kazi, na kuwa na jukumu muhimu katika kusawazisha homoni za msingi. Homoni inapokuwa hivyo, damu inaweza kuanza kunata na kusababisha mgando.
Dawa ya TRV027 - ambayo ilikuwa chanzo cha aliyeibuna kushinda tuzo ya Nobel - inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kurekebisha homoni.
Tiba nyingi ambazo zinafanyiwa majaribio ya kutibu ugonjwa wa Covid-19 zinazingatia zaidi kukabiliana na kufura kwa mwili.
Lakini kutosawazika kwa homoni ni tatizo kubwa, ambalo linaweza kutoa kidokezo katika suala la kwanini watu wengine huumwa sana wakipata Covid-19 tofauti na wengine, amesema Dkt. David Owen, kulingana na moja ya tafiti iliyofanywa.
Kuganda kwa damu kunaweza kuelezea kwanini ugonjwa wa Covid-19 unaathiri hasa watu wenye matatizo ya moyo licha ya kwamba ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumua, kulingana na Wakfu wa British Heart.


EmoticonEmoticon