Floyd Mayweather Ajitolea Kusimamia Gharama Za Mazishi Ya Mmarekani Mweusi Aliye Uliwa Na Polisi

Bondia Maarufu na Tajiri ulimwengu Floyd Mayweather amejitolea kulipia gharama zote za mazishi ya George Floyd Mmarekani mweusi aliye uliwa na polisi huko Minneapolis wiki iliyopita.

Mtandao wa TMZ umesema kwamba , tayari Mayweather ameishathibitisha na kuihakikishia familia ya Marehemu kuwa , atasimamia gharama zote za mazishi ya George Floyd.

Shughuli ya Mazishi ya George Floyd zinatazimiwa kufanyika katika miji minne tofauti ya nchini Marekani, ambayo ni Houston Texas alipozaliwa, Minnesota ambapo umauti wake ulimkuta, Charlotte na mji mwengine ambao bado haujawekwa wazi .


EmoticonEmoticon