Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi Juni 18

Leo Messi
Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Juni 18

1. Barcelona itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32, ya mkataba mpya ili kuendelea kuwa kwenye hiyo hadi 2023.

2. Mshambuliaji wa Uhispania Pedro, 32, amekubali kujiunga na Roma kwa uhamisho wa bila malipo na anatakiwa kuamua ikiwa atasaini mkataba wa muda mfupi kusalia Chelsea hadi mwisho wa msimu.

Hata hivyo, Pedro hayuko tayari kumaliza msimu na Blues kwasababu hataki kuhatarisha uhamisho wake wa Roma. 

3. Kiungo wa kati wa Scotland Ryan Fraser, 26, anataka zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki kusaini mkataba wa kuwa wakala huria baada ya kukataa ofa ya mkataba wa muda mfupi kusalia Bournemouth kwa kipindi kilichosalia msimu huu.

4. Bayern Munich itafikiria kumuuza beki wa kushoto wa Austrian David Alaba, 27, badala ya kukatiza mkataba wake.

5. Kocha Mikel Arteta ameitaka bodi ya Arsenal kumuunga mkono ili kuimarisha kikosi chake wakati wa kipindi cha usajili - baada ya mahasimu wao kwenye Ligi ya Primia Chelsea kukubali makubaliano ya pauni milioni 54 kumsaini mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka RB Leipzig. 


EmoticonEmoticon