Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Juni 12

Coutinho na Thomas Muller
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Juni 12


1. Barcelona wanamsaka beki kutoka Tottenham na Chelsea katika mkataba wa kubadilishana wachezaji utakaomjumuishwa Philippe Coutinho,27. 

2. Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller amedokeza kuwa angelipendelea kujumuika kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, ambaye anapigiwa upatu kuhama Leverkusen msimu huu wa joto.

3. Mazungumzo yanaendelea kati ya Juventus na Barcelona kuhusu mpango wa kubadilishana wachezaji wa safu ya kati utakaojumuisha Miralem Pjanic, 30, na Arthur Melo,23. 

4. Liverpool wamehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo, licha ya tetesi kuwa huenda wakawauza baadhi ya wachezaji wao wanaolipwa mshahara mku, klabu hiyo ya Serie A haina mpango wakumuuza kiungo huyo wa miaka 20.

5. Chealsea huenda ikamuuza kiungo wake wa kati N'Golo Kante, 29, kwa Real Madrid ili ipate fedha za kununua wachezaji wapya. 


EmoticonEmoticon