Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Juni 19

David Luiz, Arteta Arsenal
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Juni 19

1. Kandarasi ya mlinzi wa Brazil David Luiz na timu ya Arsenal inamalizika Juni 30 na wasimamizi wake wanasema hatma ya mchezaji huyo, 33, katika klabu hiyo itajulikana mwisho wa wiki.

Luiz anataka mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwa na Gunners lakini timu hiyo iko tayari kumuongezea mkataba wa miezi 12. 

2. Bayern Munich imekubali kuendeleza mkataba wa makubaliano ya mkopo ya mchezaji wa Brazil, Philippe Coutinho, 28, kutoka Barcelona hata zaidi ya Juni 30, ili mchezaji huyo aweze kucheza michuano ya mwisho ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Agosti.

3. Chelsea iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 29, kusaidia kukusanya pesa za uhamisho zaidi kufuatia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner kutoka RB Leipzig.

4. Arsenal na Manchester United wote wana nia ya kumsajili winga wa Roma, Cengiz Under, 22, huku winga huyo wa Uturuki akipangiwa kuwa na gharama ya pauni milioni 27.

5. Everton inaonekana kuwa tayari kutomsajili Gabriel Magalhaes, 22, kutoka Lille wakati mlinzi huyo wa Brazil akiwa amepangiwa kujiunga na upande wa Italia, Napoli.


EmoticonEmoticon