Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Juni 5

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Juni 5
1. Beki wa kushoto wa England Ben Chilwell 23, anashawishiwa na kujiunga na Chelsea baadae msimu huu lakini bado hajaomba kuondoka Leicester City .
2. Liverpool haitapambana na Chelsea kwa ajili ya kupata sahihi ya Timo Werner wakati mshambuliaji huyo,24, anayekipiga RB Leipzig yuko kwenye mpango wa kuelekea Stamford Bridge.
3. Tottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen,33, kuamua kama ataendelea kubaki mpaka msimu utakapomalizika au ataondoka kabla msimu kuisha
4. Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff hajakuwa mazoezini wiki hii wakati kukiwa hakuna uhakika kuhusu mustakabali wake kwenye klabu hiyo, huku klabu ya Udinese ya Serie A ikiripotiwa kutoa ofay a mshahara wa pauni 30,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo, 20, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu.
5. Manchester City wanatarajia kuanza mazungumzo na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Eric Garcia huku klabu yake ya zamani Barcelona ikimtaka mchezaji huyo.


EmoticonEmoticon