Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne Juni 16

Tetesi Za Soka Ulaya
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Juni 16
1. Leicester City wanapambana na Crystal Palace kuwania sahihi ya beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 27.
2. Manchester City wanamtazama kwa karibu beki wa kulia raia wa Morocco na mchezaji wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21. Kwa sasa anachezea kwa mkopo timu ya Borussia Dortmund.
3. Juventus wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho, 28, na beki wa kushoto Muhispania Marcos Alonso,29.
4. Uhamisho wa Timo Werner kutoka RP Leipzig kwenda Chelsea utakamilika rasmi juma hili, wakati mkataba wa mshambuliaji huyo wa Kijerumani wa pauni milioni 53 unakwisha leo.
5. Kiungo wa zamani wa Uholanzi Ronald de Boer amesema kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 23, angependa kuhamia Real Madrid kuliko Manchester United.


EmoticonEmoticon