Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne Juni 2

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Juni 2
1. Chelsea wanafikiria kubadili uamuzi wao kwa kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner,24, ikiwa Mjerumani huyo ataonesha nia utayari wa kuhama.
2. Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or Lionel Messi, 32, atasalia Barcelona msimu ujao baada ya kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu mshambuliaji huyo wa Argentina kuondoka baada ya mkataba kuisha msimu huu.
3. Real Madrid wamekataa nafasi ya kumsajili winga wa Chelsea Willian, 31, kwa uhamisho huru.Mkataba wa mchezaji huyo wa Brazil unamalizika msimu huu.
4. Manchester United italipa pauni milioni 10.5 kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kucheza kwa mkopo kwa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo mpaka mwezi Januari, ada ya pauni milioni 6 inakwenda Shanghai Shenhua na pauni 130,000 ni mshahara wa wiki.
5. Chelsea imepeleka mapendekezo yake kwa ligi ya primia kuongeza idadi ya wachezaji wa kubadilisha wanaoruhusiwa kuwa kwenye benchi kuwa tisa badala ya saba katika kipindi hiki cha msimu uliobaki.


EmoticonEmoticon