Habari 5 Kubwa Za Soka Jumapili Juni 7

Tetesi Za Soka Ulaya Jumapili Juni 7

1. Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewataja Havertz na Werner kama wachezaji wazuri lakini akasisitiza kwamba ujio wa virusi vya corona ndio uliozuia klabu yake kuwasaini. Pia wameulizia kuhusu winga wa Uhispania na Wolves Adama Traore, 24.

2. Barcelona imefungua kandarasi mpya na nahodha na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi ,32 na kipa wa Ujerumani Marc- Andre ter Stegen ,28 .

3. Kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, amempiku mchezaji mwenza anayeichezea Borussia Dortmund winger Jadon Sancho, 20, kama mchezaji anayelengwa sana na Manchester United mwisho wa msimu huu.

4. Chelsea itasikiza ofa za wachezaji kadhaa kutokana na kuwasili kwa winga wa Morocco na Ajax Hakim Ziyech, 27, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka klabu ya RB Leipzig mwisho wa msimu huu .

5. Mchezaji anayelengwa na Manchester United na Chelsea Federico Chiesa ameambiwa anaweza kuondoka katika klabu ya Fiorentina. Mmiliki wa klabu hiyo anasema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Italia anaweza kuondoka.


EmoticonEmoticon