Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano Juni 10

Jadon Sancho Man United
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Juni 10

1. Chelsea inaamini kwamba mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon sancho, 20, atajiunga na Man United hivyobasi inamnyatia kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz.

2. Beki wa kati wa Brazil Thiago Silva anataka kusalia barani Ulaya baada ya kuambiwa kwamba kandarasi yake katika klabu ya PSG haitaongezwa , na anaamini anaweza kuichezea timu kubwa kwa misimu miwili zaidi.

Huku Klabu tano za ligi ya Premia - Arsenal, Everton, Newcastle, West Ham na Wolves - zinafikiria kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kutoka PSG.

3. Leicester City inamlenga beki wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, kuchukua nafasi yake mchezaji wa England Ben Chilwell, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Chelsea na Manchester City. 

4. Manchester United haiko tayari kumuachilia winga wa Wales Daniel James, 22, kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo - iwapo watamsaini mchezaji wa England Jadon Sancho.

5. Aston Villa wamekuwa wakivutiwa kwa muda mrefu na mchezaji wa Algeria Benrahma mwenye umri wa miaka 24 na watajaribu kumsajili iwapo wataepuka kushushwa katika ligi ya Premia.


EmoticonEmoticon