Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano Juni 17

Jadon Sancho, Gareth Bale
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Juni 17

1. Manchester United imefanya mawasiliano na wawakilishi wa Willian kuzungumzia uhamisho huru kwa ajili ya mshambuliaji huyo, 31, ambaye mkataba wake na Chelsea umefika ukingoni msimu huu.

2. Kocha wa Everton Carlo Ancelotti ameanza mazungumzo na klabu ya zamani ya Napoli kuhusu kiungo wa Kireno Allan, 29.
Ancelotti pia anajaribu kumsajili Mbrazili anayekipiga St-Germain katika nafasi ya ulinzi Thiago Silva kwa uhamisho huru, mara tu mkataba wake utakapokwisha msimu huu. 

3. Mahusiano ya Gareth Bale na kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane yamefikia hatua ya kushindikana, lakini mshambuliajii huyu ameendelea kuwa na furaha.

4. Mustakabali wa Jadon Sancho kwenye kikosi cha Borussia Dortmund bado umekuwa si wa uhakika baada ya kocha mkuu Lucien Favre kumuorodhesha mshambuliaji huyo,20, kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuondoka msimu huu.

5. Chelsea imeongezewa nguvu katika mbio zake za kumnasa Kai Havertz huku Bayern Leverkunsen ikisema hawata 'mzuia' iwapo atataka kuondoka baada ya kiungo huyo Mjerumani, 21 kusema anahitaji changamoto mpya. 


EmoticonEmoticon