Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi Juni 25

Tanguy Ndombele
Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Juni 25

1. Mchezaji wa Tottenham aliyesaini kandarasi iliovunja rekodi ya dau la £54m Tanguy Ndombele, 23, amemwambia mkufunzi wake Jose Mourinho kwamba hataki tena kucheza chini yake. Paris St-Germain, Barcelona na Bayern Munich zote zinamnyatia kiungo huyo wa kati wa Ufaransa.

2. Barcelona itavutiwa na mpango wa kubadilishana wachezaji huku Ndombele akijiunga na timu hiyo na winga wa kulia wa Portugal Nelson Semedo, 26, au winga wa Brazil Phillipe Coutinho 28 ambaye kwa sasa yuko Bayern Munich kwa mkopo akijiunga na Spurs.

3. Juventus imeulizia kuhusu mashambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre- Emerick Aubameyang, 31, ikijiunga na Bareclona na Intermilan miongoni mwa timu zilizovutiwa na mchezaji huyo.

4. Manchester United ndio chaguo la winga wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 20. Lakini klabu hiyo ya Bundesliga haitamuachilia kwa chini ya £118m.

5. Liverpool wanapigiwa upatu kumsaini Thiago Alcantara kwa dau la £43m baada ya kiungo huyo wa Uhispania, 29, kuvunja mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake Bayern Munich


EmoticonEmoticon