Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne Juni 23

Lautaro Martinez 22
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Juni 23
1. Barcelona imehusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22 lakini afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Giuseppe Marotta anasema kwamba mchezaji huyo wa Argentina hajakuwa na hamu ya kutaka kuondoka ".
2. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta huenda akafikiria uhamisho wa bila malipo wa kipa wa England Joe Hart 33 , ambaye ataachiliwa na Burnley mwisho wa mwezi baada ya kipa wa Ujerumani Bernd Leno,28 kupata jeraha dhidi ya klabu ya Brighton.
3. Chelsea huenda ikaelekeza hamu yake ya kumsajili beki wa kushoto wa Ufaransa na PSG Layvin Kurzawa, 27 iwapo watashindwa kumsaini mchezaji wa leicester na England Ben Chilwell, 23 
4. Liverpool wamewasilisha dau la £54m kumsajili beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pia anazivutia klabu za Manchester United na Chelsea. 
5. Juventus iko tayari kuipatia wachezaji wawili wa Itali - beki Daniele Rugani, 25 na winga Federico Bernardeschi, 26 - klabu ya Wolves katika jaribio la kupunguza gharama ya kumnunua mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29.


EmoticonEmoticon