Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumapili Juni 28

Jurgen Klopp, Jadon Sancho
Tetesi Za Soka Ulaya Jumapili Juni 28

1. Borussia Dortmund wanaamini winga wao Muingereza Jadon Sancho atasalia katika klabu hiyo, kwa kuwa hawajapokea ombi lolote la kutaka kumnunua mchezaji huyo.

2. Jurgen Klopp amekiri kuwa Sancho "atapendeza sana" akivalia jezi ya Liverpool, lakini mkufunzi huyo hajagusia ikiwa klabu hiyo ina mpango wa kumnunua mchezaji yeyote msimu huu wa joto.

3. Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hajakataa wala kuthibitisha ikiwa Sancho atahamia klabu hiyo msimu wa joto dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa.

4. Mabigwa wapya wa ligi ya Premia, Liverpool wanajiandaa kumnunua beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 29, katika siku chache zijazo.
5. Chelsea wanapania kumsajili kipa wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 24, kuchukua nafasi ya Kepa Arrizabalaga. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 25-amehusishwa na uhamisho wa kuenda Valencia msimu huu wa joto kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili. 


EmoticonEmoticon