Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Juni 24

Arthur Barcelona Juventus
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Juni 24

1. Juventus imekubali dau la euro milioni 80 na Barcelona kumsaini mchezaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 Arthur - lakini bado watalazimika kumshawishi kiungo huyo kujiunga nao.

2. Kiungo wa kati wa Portugal William Carvalho, 28, ameafikia makubaliano na klabu ya Leicester City , huku klabu hiyo ya Premia ikihitaji kukubaliana dau la uhamisho na klabu ya Real Betis.

3. Kiungo wa kati wa Manchester United na England lder Dion McGhee, 19, ananyatiwa na West Ham, Rangers na AZ Alkmaar.

4. Crystal Palace inakaribia kumsaini Nathan Ferguson baada ya West Brom kuthibitisha kwamba beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 19 alikataa kutia saini kandarasi mpya.

5. Mamlaka ya soka nchini England inatafuta njia ya kutumia kombe la Community Shield kama jaribio la kurudi kwa mashabiki kabla ya kuanza kwa msimu ujao.


EmoticonEmoticon