Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne Juni 30

 Jack Grealish
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Juni 30

1. Manchester City itafikiria kumsajili kiungo wa kati Jack Grealish , 24 , ikiwa Bayern itamnunua winga wa Kijerumani Leroy Sane,24. Manchester United pia wamehusishwa na habari ya kumsajili Muingereza huyo.

2. New Castle na Arsenal ni miongoni mwa klabu za primia ambazo zinapenda kumsajili mshambuliaji wa Kiholanzi anayekipiga Wolfsburg Wout Weghorst,27 kwa kitita cha pauni milioni 35.

3. Wachezaji wanaolengwa na Chelsea, mlinda mlango wa Cameroon, Andre Onana 24, na beki wa kushoto Nicolas Tagliafico,27 wameambiwa wanaweza kuondoka Ajax.

4. Mchezaji wa nafasi ya ulinzi ndani ya Paris St-Germain Layvin Kurzawa amesaini mkataba wa miaka mine na klabu hiyo . Mfaransa huyo ,27, alihusishwa na taarifa za kuchukuliwa na Arsenal na Liverpool. 

5. Mabingwa wa ligi ya Primia, Liverpool hawatatumia 'mamilioni ' kwenye soko la uhamisho, amesema kocha Jurgen Klopp.


EmoticonEmoticon