Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu Juni 29

Kalidou Koulibaly
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu Juni 29

1. Liverpool wameripotiwa kuwa wako mbele ya Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati-nyuma Msenegal Kalidou Koulibaly, 29, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Napoli kwa kumtoa Mcroasia Dejan Lovren, anayecheza safu ya ulinzi akiwa na umri wa miaka 30, kama sehemu ya uhamisho. 

2. Chelsea imepata msukumo wa uhamisho kwa meneja wa Ajax - Erik ten Hag kupendekeza kuwa difenda wa Argentina Nicolas Tagliafico mwenye umri wa miaka 27 na mlindalango wa Cameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 24, wanaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu huku kiungo wa kati wa Uholanzi Donny Van de Beek, anayelengwa na Manchester United akisemekana lkuwa huenda pia akaondoka katika klabu hiyo.

3. Manchester City wamejipanga kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus Muhispania Pablo Moreno, mwenye umri wa miaka 18, katika dili ya kubadilishana mchezaji huyo ambayo itamuwezesha winga Felix Correia, mwenye umri wa miaka 19, kuhamia upande mwingine.

4. Inter Milan wanaangalia uwezekano wa kumuuza Mslovakia difenda Milan Skriniar, 25, msimu huu huku Manchester City wakiwa ni miongonbi mwa wale wanaomtaka. Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa City Muargentina Sergio Aguero, 32, anaweza kuwa sehemu ya kuweno katika mkataba huo . 

5. Mkurugenzi mkuu wa wakurugenzi Giuseppe Marotta anasema kuwa " mazungumzo ya klabu yamefikia kiwango cha juu" kwa ajili ya mchezaji wa Borussia Dortmund anayecheza kwa mkopo Achraf Hakimi huku beki wa huyo wa Real Madrid Mmorocco , 21, na kikaribia kuwa na uwezekano wa kuhamia serie A.


EmoticonEmoticon