Hofu Ya Janga La Homa Ya Mafua Laibuka China

nguruwe
Ugonjwa mpya wa mafua ambao unauwezekano wa kuwa janga umetambuliwa nchini China na wanasayansi.

Mlipuko huo umejitokeza hivi karibuni na upo miongoni mwa nguruwe lakini hata binadamu wanaweza kuambukizwa, wameeleza wanasayansi.

Watafiti wana wasiwasi kuwa hali inaweza kubadilika na kuweza kusambaa kiurahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na kusababisha mlipuko wa ugonjwa duniani.

Wanasema tatizo hili si kwamba litatokea kwa haraka, lakini kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi kuambukiza binadamu na hivyo kuna uhitaji wa ufuatiliaji wa karibu.
Kwa sababu ni ugonjwa mpya, watu watakuwa hawana kinga ya virusi hivyo au iko kidogo.

Wanasayansi wameandika katika jarila la ' Proceedings of the National Academy of Sciences' kuwa hatua za kukabiliana na virusi hivi vya nguruwe ni kufuatilia kwa karibu wafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vya nguruwe na utekelezaji ufanyike kwa haraka.


EmoticonEmoticon