Nicki Minaj Atangangaza Mwendelezo Wa Ujio Wa Album Yake Mpya

Nicki Minaj
Huwenda ujio wa Nicki Minaj ukawa ni mwendelezo wa album yake ya kwanza, ameanza kudokeza jina ambalo linatafsiriwa kama ndio title ya album yake ijayo.

Kupitia twitter jana Minaj aliandika "PF2" neno ambalo limetafsiriwa kama (Pink Friday 2) kumbuka Pink Friday ni album ya kwanza ya Nicki Minaj ambayo ilitoka na kumtambulisha mwaka 2010.
Nicki Minaj Tweet
The Queen kutoka New York, mnamo Februari 8 mwaka huu, alitupasha kwamba tayari amelikamilisha jina la album yake. "I have the title already"

Mara ya mwisho kwa Minaj kutubariki na album ilikuwa Agosti, 2018 alipoachia "Queen" album yake ya Nne.


EmoticonEmoticon