Huyu Ndiye Mrembo Mpya Anayetoka Na Rapa Lil Wayne Kwa Sasa

Denise Bidot & Lil Wayne
Baada ya kuachana na mrembo La'Tecia Thomas, Lil Wayne anaonekana anapenda sana wasichana wanamitindo, ametajwa kutoka kimapenzi na mwanadada mrembo mwenye asili ya Puerto Rico-Kuwait aitwaye Denise Bidot.

Uvumi wa wawili hawa kuwa kwenye mahusiano ulianza pale ambapo Wayne alionekana kum-follow mrembo huyo pekee kwenye instagram. Pia siku ya Ijumaa (June 12) wakati akipiga stori na Nicki Minaj kwenye Young Money Radio, alimwambia kuwa sasa ana mpenzi mpya kwenye maisha yake.
Denise Bidot
Denise ni mwanamitindo ambaye amefanya kazi na makampuni mbali mbali kama Savage x Fenty, Lane Bryant na Levi's. Pia amepita kwenye majukwaa makubwa ya maonesho ya mitindo kama New York Fashion Week.


EmoticonEmoticon