Irani Imetoa Idhini Ya Kukamatwa Kwa Raisi Wa Marekani Donald Trump

Verified

Iran imetoa waranti ya kukamatwa na imeliomba msaada Shirika la Polisi ya Kimataifa Interpol kumkamata Rais Donald Trump na wengine kadhaa inaoamini walifanya shambulio la ndege isiyo na rubani lililomuuwa jenerali wa juu wa Iran mjini Baghdad.

Mwendesha mashtaka wa Iran Ali Alqasimehr amesema Trump na Watu wengine zaidi ya 30 ambao Iran inawatuhumu kwa kushiriki katika shambulio la Januari 3 lililomuuwa Jenerali Qassem Soleiman mjini Baghdad, wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya ugaidi.
Iran haijawataja wengine wanaotafutwa zaidi ya Trump, lakini wamesisitiza kuwa Iran itaendelea kufuatilia mashtaka dhidi yake hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa urais.

Shirika la Interpol lenye makao yake nchini Ufaransa, halikujibu maombi ya kuzungumzia suala , mashtaka hayo yanaonyesha mzozo unaozidi kati ya Iran na Marekani tangu Trump alipoitoa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa makubwa.


EmoticonEmoticon