Jarida La Forbes Limetoa Orodha Ya Mastaa Wanaoingiza Mkwanja Mrefu 2020

Binti mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa Los Angeles California nchini Marekani, Kylie Jenner ametajwa kukamata namba 1 kwenye orodha ya watu maarufu 100 ambao wamelipwa/wametengeneza pesa nyingi kwa mwaka 2020 kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Kwenye orodha hiyo (The World's Highest Paid Celebrities) Kylie Jenner ambaye hivi karibuni utajiri wake wa hadhi ya bilionea ulitiliwa mashaka na Forbes, ametajwa kutengeneza kiasi ($590M) sawa na Trlioni 1.3 za Kitanzania katika kipindi cha mwaka mzima, kuanzia Juni 2019 hadi Juni 2020 ambapo kipato kikubwa kimetokana na kuuza asilimia 51 ya hisa za kampuni yake (Kylie Cosmetics) kwa Coty mwezi Januari mwaka huu.

Namba mbili kwenye orodha hiyo imekaliwa na shemeji yake Kylie, rapa Kanye West ambaye ametengeneza kiasi cha ($170M) sawa na bilioni 393.8 za Kitanzania, mapato yake yakitajwa kuwa nje ya muziki na kuingia kupitia kampuni yake YEEZY ambayo ina dili na biashara za Viatu na mavazi.

HII HAPA TOP 10 (Kabla ya kukatwa kodi)
1. Kylie Jenner - $590M
2. Kanye West - $170M
3. Roger Federer - $106.3M
4. Cristiano Ronaldo - $105M
5. Lionel Messi - $104M

6. Tyler Perry - $97M
7. Neymar - $95.5M
8. Howard Stern - $90M
9. LeBron James - $88M
10. Dwayne Johnson - $87.5M

Mwafrika pekee ambaye ameingia kwenye orodha hii ni nyota wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah wa Misri, ameingiza kiasi cha ($35.1M) sawa na Bilioni 82 za Kitanzania.

Forbes wanadai mapato ya watu wote mashuhuri kwa ujumla ni ($6.1B) sawa na Trilioni 14.1 za Kitanzania kabla ya kukatwa kodi na ada, ambalo ni anguko la ($200M) kutoka kwa mwaka 2019, hii ni baada ya mlipuko wa janga la Corona kusimamisha viwanja na matamasha duniani kote.


EmoticonEmoticon