Justin Bieber Afunguka Kushawishiwa Na Tamaduni Za Watu Weusi

Justin Bieber
Ni takribani wiki mbili tangu mauaji ya George Floyd ambaye ameamsha hisia kwa jamii ya watu weusi nchini Marekani na dunia kwa ujumla kwa kuanza kudai usawa.

Sio tu jamii ya watu weusi pekee ambayo imetoka na kuandamana, hata wazungu nao wamejitokeza akiwemo Justin Bieber ambaye ameonekana kupitia ukurasa wake akihamasisha dhidi ya usawa na kampeni ya Black Lives Matter.

Justin Bieber amesema asilimia kubwa ya mafanikio yake na muziki wake yamechagizwa na tamaduni za watu weusi kuanzia mtindo wa uimbaji, kunengua, kutumbuiza na hata mitindo.

"Nimeshawishiwa na tamaduni za mtu mweusi. Nimefaidika kupitia tamaduni zao. Mtindo wangu, namna ninavyo imba, nengua, kutumbuiza na hata mitindo ya mavazi yote hayo yamechagizwa na kusukumwa na tamaduni za mtu mweusi." aliandika JB kwenye IG yake.


EmoticonEmoticon