Kanye Atoa Bil. 4.6 Kumsomesha Mtoto Wa George Floyd

Ikiwa ni saa chache kupita baada ya kutangazwa na Forbes kuingiza kiasi cha Tsh Bilioni 393.8 kwa mwaka 2020, na kuwa kinara kwa wasanii, Kanye West, ameingia  kwenye headlines   za vyombo vya habari kwa mara nyingine ambapo ameripotiwa kuchangia kiasi cha $2M ambazo sawa na takribani Tsh. Bilioni 4.6 kwenye familia za George Floyd, Breonna Taylor na Ahmaud Arbery.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, pesa hiyo yote imeenda kuchangia mfuko  kwa ajili ya masomo uitwao ‘529 College Savings Plan’ ili kumsaidia binti wa marehemu George Floyd, aiwaye Gianna (6) kulipa ada ya shule. Mbali na hilo, Kanye pia amechangia  gharama za kuendesha kesi, kwa familia hiyo.


EmoticonEmoticon