Kendrick Lamar Ajiunga Na Waandamanaji Kutetea Haki Za Watu Weusi

Kendrick Lamar
Hatusikii kazi mpya kwa miaka sasa, hatumuoni jukwaani, wala mitandaoni lakini kwenye maandamano ya kushinikiza juu upatikani wa usawa na kupinga ukatili wa polisi dhidi ya watu weusi, rapa Kendrick Lamar amejitokeza.

K-Dot alionekana juzi Jumapili kwenye mitaa yake ya Compton akiwa amekula bati huku amevalia hoodie nyeusi na mask. Aliongozana pia na DeMar DeRozan na Russell Westbrook kuikata mitaa ya Gateway Town Center hadi Martin Luther King Jr. monument.


EmoticonEmoticon