Kenya Yasajili Visa Vipya 117, Jumla 4,374

Wizara ya Afya Kenya
Katibu katika wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema watu 117 wamepatikana na virusi vya corona huku wakenya wakiwa 112 na watu wa kigeni wakiwa 5.

Kutokana na takwimu hizo mpya, Kenya sasa ina watu 4,374 walioambukizwa virusi hivyo.
Kaunti ya Nairobi imesajili visa 52 huku Mombasa ikiwa 22, Kajiado 18.

Watu wengine 91 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 1,550 waliopona.

Wagonjwa wengine wawili wamefariki na kufikisha watu 119 waliokufa kutokana na virusi hivyo.

Aman amewataka kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali kama njia ya kupunguza maambukizi.

Katika kaunti ya Nairobi visa hivyo vimetokea maeneo yafuatayo,Kibra 8,Lang’ata 8,Dagoreti north ,6,Makadara 6,Embakasi east 4,Embakasi  north 3,Embakasi south 3,Mathare 2,Ruaka 2,Embakasi central 2,Embakasi west 1,Starehe 1,Kasarani 1.

Visa 22 kaunti ya Mombasa vimetokea maeneo ya Mvita 8,Kisauni 5,Changamwe 4,Likoni 3,Jomvu 1,Nyali 1.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon