Kiongozi Wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Asema Corona Imefichua Unafiki

Papa Francis
Papa Francis anasema janga la virusi vya corona limeonyesha ni kwa jinsi gani maskini wametengwa na jamii.
Mara nyingi umaskini umekua ukifichwa, anasema, lakini kujaribu kuwasaidia wengine kunaweza kutusaidia kujitambua wenyewe.
''Mzozo huu wa virusi vya corona unatuathiri sisi sote, tajiri na maskini, na kuonyesha wazi unafiki, nina wasiwasi baadhi ya wanasiasa wanaoongea kuhusu jinsi wanavyokabiliana na mzozoz huu, kuhusu njaa duniani, lakini wakati huo huo wanatengeneza silaha'',amesema Papa katika mahojiano maalum na BBC.
Ameongeza kuwa huu ni wakati wa kuondokana na aina hii ya unafiki katika utendaji. Vinginevyo uachane na imani zetu au tutapoteza kila kitu.
Papa Francis anasema kila mzozo una hatari na fursa kwa pamoja. Leo nina imani kuwa tunapaswa kupunguza kiwango cha uzalishaji na ulaji na kujifunza kuelewa na kuitazama kwa makini duniahalisi. 
Tunahitaji kuwasiliana tena na mazingira yetu huu ndio wakati wa kuwa na mabadiliko.
''Ninaona uchumi ambao ni wa kiutu zaidi. Lakini tusipoteza kumbukumbu zetu tena pale janga hili litakapoisha,tusifunike yote yaliyotokea na kurejea tena tulikotoka '',amessema Papa 
Ameongeza kuwa huu ni wakati wa kuchukua hatua za kimaamuzi, za kuachana na matumizi au kutumia vibaya mazingira wakati yote haya yatakapoisha. 
Amewataka wakazi wa dunia kutafakari na kushukuru kwa mali asili za dunia .''Tumepoteza hali ya kutafakari; tunapaswa kurejea nyuma, amesema.


EmoticonEmoticon