Kiwango Cha Dhamana Ya Kuwaweka Nje Askari Walioshirika Mauaji Ya George Floyd Chawekwa Wazi

Jaji wa mahakama ya mjini Minneapolis ameweka kiwango cha dhamana kwa waliokuwa maofisa wa polisi ambao wanashtakiwa kwa mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd.

Jana alhamis Jaji aligonga nyundo na kusema washtakiwa hao watatu watatakiwa kulipiwa dhamana ya ($1 Million) takribani TSH. Bilioni 2 kwa kila mmoja, ili kuwa nje ya gereza kwa kipindi hiki cha usikilizwaji wa kesi yao.

J. Alexander Kueng, Thomas Lane na Tou Thao walifikishwa mahakamani jana ikiwa ni siku moja baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji kwa kusaidia na kukimbilia katika kukamata kitendo kilichopelekea mauaji ya George Floyd.

Shauri lao litatupiwa tena sikio Juni 29 mwaka huu.


EmoticonEmoticon