Korea Kaskazini Imetishia Kutuma Jeshi Eneo Salama La Mpakani

Jeshi la Korea Kaskazini
Jeshi la Korea Kaskazini limeonya kwamba liko tayari kuingia katika eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi linalogawanya nchi hiyo na Korea Kusini.
Tishio hilo linatokana na makundi yaliyoasi na kutorokea Korea Kusini yanayosambaza propaganda Korea Kaskazini.
Wikendi, Kim Yo-jong, dada ya kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un, alisema kwamba ataagiza jeshi kuelekea eneo.
Na sasa hivi jeshi linasema liko tayari kubadilisha eneo hil kuwa ngome yao na kugusia kuwa liko macho.
Wasiwasi kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiongezeka kwa muda sasa kwasababu ya vipeperushi ambavyo vimekuwa vikisambaa katika mpaka wa maeneo hayo mawili ambavyo kawaida huwa vinatumwa kwa njia ya maputo.
Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Jumanne amejibu vitisho hivyo kwa kusema kuwa inashirikiana na Marekani kufuatilia kwa karibu hatua za kijeshi upande wa Korea Kaskazini.


EmoticonEmoticon