Lazarus Chakwera Aapishwa Kuwa Rais Mpya Wa Malawi

Lazarus Chakwera
Hafla ya kumuapisha Lazarus Chakwera kuwa rais mpya wa Malawi zinaendela muda huu baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Alimshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa asilimia 58.57 ya kura katika uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.
Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.
Nchi iligawanyika vikali wiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio.

Malawi ni nchi ya kwanza Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuandaa duru ya pili ambayo upinzani ukanyakua ushinda.
Kama ilivyotokea Malawi nchini Kenya upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 na kushinda mahakamani.
Hata hivyo mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia duru ya pili ya uchaguzi.
Baada ya matokeo rasmi kutangazwa usiku wa Jumamosi, Bw. Chakwera alisema ushindi wake ni "ushindi wa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."

Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za magari na wengine wakipiga fataki.


EmoticonEmoticon