Licha ya Corona Marekani, Trump azindua kampeni ya kuwania Urais mwezi Novemba

Trump wa Marekani amezinduwa kampeni
Rais Donald Trump wa Marekani amezinduwa kampeni yake kuwania kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi wa Novemba, kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara, licha ya kitisho cha virusi vya korona, katika mji wa Tulsa.

Trump ameutumia mkutano huo kuwashambulia wapinzani wake wa Democratic. Aidha aliutumia mkutano huo wa mjini Tulsa, jimbo la Oklahoma uliokuwa umepigiwa debe, kuiimarisha kampeni yake inayoyumba wakati kukiwa na janga kubwa la kiafya na mgogoro wa kiuchumi pamoja na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi ambayo yamelifagia taifa ghilo katika wiki za karibuni.
Trump wa Marekani amezinduwa kampeni
Mrepublican huyo amedai ushindi dhidi ya janga hilo ambalo limewauwa karibu Wamarekani 120,000 – “Nimefanya kazi nzuri sana nao!” – hata wakati watu sita wa timu yake ya kampeni wakipatikana na maambukizi ya COVID-19.
Trump alimshambulia mpinzani wake katika uchaguzi wa 2020, Mdemocrat Joe Biden, akimtaja kuwa “kibaraka wa watu wa siasa kali za mrengo wa kushoto.”
Rais huyo alipuuza kitisho kuwa mkutano huo wa jioni – huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliohudhuria – huenda ukachochea mlipuko mpya wa virusi vya corona, na kupuuza onyo lililotolewa la maafisa wa afya wa Tulsa na manispaa ya mji huo.


EmoticonEmoticon