Magavana Wampinga Trump Kwa Kauli Yake Ya Kutuma Jeshi Kutuliza Ghasia

Wakati maandamano yakishika kasi nchini Marekani, Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ametishia kutuma majeshi yake ili kutuliza ghasia.

Bwana Trump amesema atatuma vikosi vyake kama miji na majimbo yatashindwa kutatua tatizo.
''Kama mji au jimbo litakataa kuchukua hatua ambazo ni muhimu...basi nitatuma jeshi la Marekani'', alisema rais Trump.

Lakini magavana wa majimbo wamesema serikali haina mamlaka ya kupeleka vikosi bila ridhaa ya mamlaka za majimbo.


EmoticonEmoticon