Marekani Yasitisha Matumizi Ya Dawa Ya hydroxychloroquine Kutibu Corona

hydroxychloroquine
Matumizi ya dharura ya dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria ya hydroxychloroquine kama tiba ya virusi vya corona yamefutwa kulingana na Shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA).
Shirika la (FDA) limesema kwamba ushahidi mpya kutoka kwa taasisi za afya umeonesha kuwa hakuna haja ya kuendelea kutumia dawa hiyo kwa matumaini kwamba inaweza kukabiliana na ugonjwa wa virusi.
Rais Donald Trump alitetea matumizi ya dawa hiyo ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa Covid-19.
Machi, Shirika la FDA lilitoa idhini ya matumizi ya dawa hiyo kwa wagonjwa ambao watakuwa wanaumwa sana.
Lakini Jumatatu, shirika hilo lilisema kwamba utafiti wa kwenye taasisi ulipendekeza kwamba dawa ya hydroxychloroquine haina ufanisi kwa kutibu ugonjwa huo wa virusi na kushindwa kuzuia maambukizi miongoni mwa waliopata maambukizi.
Akijibu uamuzi uliochukuliwa na Shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA), Trump alisema yeye amekuwa dawa hiyo kama kinga na hakupata madhara yoyote.
"Niliinywa na nikahisi vizuri," aliwaambia wanahabari Jumatatu, na kuongeza: "Sina malalmishi kuhusu dawa hiyo, niliinywa kwa wiki mbili, na niko hapa, tuko hapa sote."
Rais huyo, 74, alisema kwamba watu wengi walimwambia kwamba dawa hiyo imenusuru maisha yao.


EmoticonEmoticon