Mashabiki Wa Kendrick Lamar Watupiwa Lawama Kutodhamini Kazi Za Msanii Huyo

Kendrick Lamar
Licha ya mengi ambayo ameyafanya hadi sasa kwenye ulimwengu wa Hip Hop, Kendrick Lamar ameonekana kutopewa heshima anayostahili na mashabiki wake. Hii ni kwa mujibu wa meneja wake, Punch.

Akijibu tweet ya shabiki mmoja ambaye alitaka Kendrick Lamar arejee kwenye muziki, Punch aliandika "Hapana. Watu hawathamini."
Tweets ya meneja wa Kendrick
Haifahamiki ni lini K-Dot atarejea kwenye muziki baada ya kupumzika kwa takribani miaka mitatu, lakini tetesi zinasema kwamba kwa sasa anarekodi album na inatarajiwa kuachiwa muda wowote mwaka huu.


EmoticonEmoticon