Matokeo Ya Uchunguzi Wa Maiti Ya George Floyd Yabaini Kilichopelekea Kifo Chake

George Floyd, raia mweusi wa Marekani ambaye kifo chake kimesababisha maandamano makubwa Marekani, alikufa kutokana na ukosefu wa hewa safi ya (oksijeni), kwa mujibu wa uchunguzi binafsi wa maiti yake.
Alifariki kwa kukandamizwa kwa goti shingoni na mgongoni na maafisa wa polisi wa Minneapolis, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini hilo.
Matokeo hayo yanatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na madktari wa kaunti.
Kulingana na matokeo hayo, hakukupatikana ushahidi wowote unaohusisha ukosefu wa hewa wala kunyongwa.
Matokeo ya uchunguzi huo wa kimatibabu pia yalibaini kwamba matatizo ya afya yalichangia pakubwa kifo cha Bwana Floyd.
Lakini madaktari waliosimamiwa na familia ya Floyd walibaini kwamba kifo chake kilikuwa ni mauaji, taarifa kutoka kwa timu yake ya sheria inasema.
"Sababu ya kifo kwa maoni yangu kimesababishwa na ukosefu wa hewa, kutokana na kukandamizwa shingoni ambako kunaweza kutatiza oksijeni inayokwenda kwenye ubongo - na kupelekea mkandamizo mgongoni, ambako kuna tatiza upumuaji," Dkt. Michael Baden, aliyekuwa daktari wa mji wa New York pamoja na mwengine wamesema katika mkutano na wanahabari.


EmoticonEmoticon