Mauaji Ya George Floyd :Maelfu Wajitokeza Marekani Kushiriki Mandamano Usiku Kucha

Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo.
Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko.
Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali.
Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku.
Waandamanaji katika mji wa New York pia nao walikiuka hatua ya kutoka nje iliyowekwa kuanzia saa mbili usiku.
Meya wa mji alisongeza mbele muda huo kwa usiku wa pili mfululizo baada ya waandamanaji kupora eneo la kibiashara la Manhattan Jumatatu.
Na katika mji wa Washington DC, kundi kubwa la watu limeendelea kukusanyika nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa moja usiku.
Aidha, Takriban wanajeshi Taliban1,600 wamepelekwa katika maeneo ya mji wa Washington DC.


EmoticonEmoticon