Mke Wa Dr Dre Ataka Talaka Baada Ya Miaka 24 Ya Ndoa

Dr Dre
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , Nicole Young , ambe ni mke wa gwiji wa muziki wa HipHop na Mfanyabiashara Dr Dre , amefungua madai rasmi ya Kudai talaka baada ya kua pamoja kwa Miaka 24 Kwenye ndoa

Dr. Dre na Nicole walifunga ndoa mwaka 1996 na wamebarikiwa kupata watoto wawili wakiume na wa kike ambao ni vijana kwa Sasa , Truice na Truly

Kwa mujibu wa chanzo Cha karibu na familia hiyo , kinasema kuwa bado madai hayo yapo Kwenye hatua za mwanzo , lakini Mwanamama huyo atadai fidia za talaka hiyo kutoka kwa Dr Dre ambae ana utajiri wa Dola za Kimarekani million 800 (zaidi ya Trilion 1 za kitanzania)

Hivyo kwa maneno rahisi tunaweza sema , Kama Nicole akifanikisha talaka hiyo, basi atakua Bilionea kwa kiasi Cha pesa atakacholipwa Kama fidia


EmoticonEmoticon