Mkuu Wa Jeshi La Marekani Aomba Radhi Kwa Kuandamana Na Donald Trump

Donald Trump Akiongozana na mkuu wa jeshi
Mkuu wamajeshi nchini Marekani amekiri kuwa alikosea kuungana na Rais Donald Trump wakati wa alipotembea kuenda kanisa lililopo karibu na Ikulu ya Marekani ambalo liliharibiwa na waandamanaji.
Tukio hilo la Juni tarehe moja na ambalo lilizua utata lilionesha "taswira kwamba jeshi linajihusisha na siasa za ndani ya nchi", Jenerali Mark Milley alisema.
Bwana Trump alitembea hadi kanasa hilo na kupiga picha akiwa ameshikilia Bibilia baada ya maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd kuvunjwa kwa nguvu.
Trump akiwa ameshika Biblia
Hatua ya kutumia wanajeshi kukabiliana na waandamanaji imezua mjadala mkali cnini Marekani.
Trump mara kwa mara alitumia maneno "Utawala wa sheria", kuleta kikosi malum cha ulinzi katika mji mkuu wa Marekani, na kuapa kuwa atawapeleka wanajeshi katika miji mingine ya Marekani huku akilaani maandamano ya vurugu yaliyoshuhudiwa nchini humo.
Baadhi ya maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd mjini Minnepolisi mwezi uliyopita, mwanzoni yalikuwa ya amani lakini baadaye yalikumbwa na vurugu na wizi katika miji tofauti.
Lakini tangu maafisa wanne waliohusika na mauaji hayo kufunguliwa mashitaka, maandamano hayo yamekuwa ya amani, huku wanaharakati wa kimataifa wakiungana kupinga mateso ya polisi na ukosefu wa usawa katika jamii.


EmoticonEmoticon