Mmarekani Mweusi Mwingine Auawa, Maandamano Yapamba Moto, Mkuu Wa Polisi Ajiuzulu

Maandamano Atlanta

Verified

Mkuu wa Polisi wa Atlanta nchini Marekani amejiuzulu jana Jumamosi ikiwa ni saa chache baada ya Mmarekani mwingine mweusi kuuawa, kwa kupigwa risasi na Polisi wakati walipokuwa wakijaribu kumfanyia kipimo cha kubaini ikiwa ametumia kilevi.

Maafisa hao walisema Mwanaume huyo alikwapua bastola ya ganzi kutoka kwa Polisi mmoja na alipigwa risasi wakati alipokuwa akikimbia.

Mauaji ya Rayshard Brooks aliyekuwa na umri wa miaka 27 yamechochea wimbi jipya la maandamano Atlanta, baada ya wimbi la maandamano yaliyosababishwa na kifo cha George Floyd mjini Minneapolis.

mgahawa wa Wendy
Meya wa Atlanta Keisha Lance Bottoms alitangaza kujiuzulu kwa Mkuu wa Polisi jana Jumamosi wakati watu wapatao 150 walipoandamana nje ya mgahawa wa Wendy ambako kijana huyo aliuawa Ijumaa jioni, ametangaza pia kufutwa kazi kwa Polisi aliyefyatua risasi.


EmoticonEmoticon