Mwanamume Akamatwa Kwa Kuwabaka Wanawake 40 Nigeria

Ubakaji Nigeria
Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtu wanayedai kuwa amewabaka wanawake 40 katika mji mmoja katika kipindi cha mwaka mmoja .

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Abdullahi Haruna, mtu huyo alikamatwa baada ya mwanamke mmoja katika mji wa Dangora kaskazini mwa Nigeria kumpata akiwa amejificha katika chumba cha watoto kulala. 

Bw. Haruna aliongeza kuwa mtu huyo alijaribu kutoroka lakini majirani walimkimbiza na kumshika.

Chifu kiongozi wa mji huo, Ahmadu Yau, alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua muhimu kuelekea kukabiliana na uhalifu huo.

"Watu wa Dangora wanafurahia sana hatua zilizochukuliwa na tunatumaihaki ya itatekelezwa."

Wakaazi waliambia BBC kwamba mwaka jana waliishi kwa uwoga,hata ndani ya nyumba zao, kwa sababu walidokezewa wabakaji wanaruka ua na kuingia majumbani kuwabaka wanawake.

"Sasa tunaweza kufunga macho na kulala kwa amani," mmoja wa wanawake aliambi BBC.


EmoticonEmoticon