PICHA : Mwili wa George Floyd Ulivyoagwa, Askari Walipigia Magoti Jeneza

Kutoka Chuo Kikuu cha North Central mjini Minneapolis, Marekani imefanyika Ibada ya kuuaga mwili wa George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi na kusababisha maandamano makubwa Marekani na Nchi nyingine.
”Askari wamepiga magoti wakati jeneza likiingia ukumbini”
Ibada hiyo ya kumbukumbu imeongozwa na Mwanaharakati wa haki za kiraia Mchungaji Al Sharpton, ilikuwepo Familia ya Floyd, lakini pia Gavana wa Minnesota Tim Walz, Seneta wa Minnesota Amy Klobuchar na Meya wa Minneapolis Jacob Frey ni miongoni mwa waliofika katika tukio hilo la heshima .
Watu waliokusanyika kutoa heshima zao wamekaa kimya kwa Dakika 8 na sekunde 46, muda ambao Derek anadaiwa kuutumia kumkanyaga Floyd shingoni, Mastar kibao wamehudhuria akiwemo Ludar Cris, Kevin Hart na Tiffany Haddish .


EmoticonEmoticon