Polisi Watatu Waliokuwepo Eneo La Tukio Wakati Mauaji Ya George Floyd Washtakiwa

Hatimae askari Polisi watatu waliokuwepo eneo la tukio wakati George Floyd anauliwa na Polisi mwenzao , wamekamatwa na kufunguliwa Mashitaka Kuhusiana kifo chake.

Tayari Derek Chauvin , Askari ambae alimkandamiza na goti George mpaka kupelekea umauti kumkuta , ameisha kamatwa na kufunguliwa kesi ya Mauaji.

Lakini Maelfu ya waandamanaji huko Marekani, waligoma Kusitisha maandamano mpaka Askari wote watatu waliosalia wakamatwe, kwasababu walikuwepo eneo la tukio na wakashindwa kuzuia.


EmoticonEmoticon