Rais Pierre Nkurunziza Afariki Dunia

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55) amefariki Dunia
Aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55) amefariki Dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni shambulio la moyo leo Juni 9, 2020. 

Serikali ya Burundi imethibitisha kifo cha kiongozi huyo. Hivi karibuni mkewe, Denise Bucumi alilazwa nchini Kenya kwa matibabu ya #COVID19.

Kulingana na msemaji wa serikali, balozi Willy Nyamitwe, Rais Pierre Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa. 

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezo na ametuma salamu za ramirambi kwa familia.

Rais Pierre Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1963 mwanasiasa wa Burundi ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005. 

Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi.

2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu ofisini. 

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.

Zaidi ya miezi miwili kulitokea maandamano ya kumpinga Nkurunziza ambayo yaliandamana na ghasia na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 100. 

Mei 13, 2015, jaribio la mapinduzi dhidi ya Nkurunziza lilitokea akiwa nje ya nchi hiyo.

Mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare alidai kwamba amemng’oa mamlakani Nkurunziza lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walikanusha madai hayo.


EmoticonEmoticon