Raisi Wa Marekani Aomba Msaada China Ili Kushinda Awamu Ya Pili Ya Uchaguzi Wa Uraisi

John Bolton na Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump alijaribu kuomba msaada wa rais wa China Xi Jinping ili kushinda awamu ya pili ya urais, mshauri wa zamani wa Trump wa Usalama wa Taifa John Bolton ameeleza katika kitabu chake kipya.
Bolton amesema Trump aliitaka China kununua bidhaa za chakula kutoka kwa wakulima wa Marekani, kwa mujibu wa maelezo ya awali ya kitabu ambacho kimeanza kuchambuliwa na vyombo vya habari nchini Marekani.
Mwandishi wa kitabu pia anasema Trump "alisalia kuwa mbumbumbu wa namna ya kuendesha ikulu ya White House". Serikali ya Trump inajaribu kuzuia kitabu hicho kuingia sokoni.


EmoticonEmoticon