Raisi Wa Marekani Atuma Video Ya Ubaguzi Wa Rangi Mtandaoni

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma video mtandaoni inayoonyesha mmoja wa wafuasi wake akipaza sauti na kusema "nguvu ya wazungu".

Mfuasi wake huyo alikua miongoni mwa kikundi cha watu waliokua wakishiriki mkutano wa kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump katika makazi ya kustaafu yaliyoko Florida.
Picha hiyo ya video ilionyesha wafuasi na wapinzani wa rais wakilumbana na kutupiana matusi.
Bwana Trump amekanusha shutuma kwamba anataka kupata umaarufu kupitia hali ya wasi wasi iliyopo kutokana na ubaguzi wa rangi nchini humo . Msemaji wake anasema hakusikia maneno "white power" katika video
Katika ujjumbe huo wa twitter, ambao baadae ulifutwa, rais aliwashukuru aliowaita "watu wazuri wa Vijijini " - akimaanisha watu waliostaafu wanaoishi Kaskazini-magharibi mwa Orlando ambako mkutano huo wa kampeni ulifanyika . "Wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto hawafanyi lolote Democrats wataangushwa . Mfisadi Joe amepigwa . Tuonane hivi karibuni !!!," aliandika.
Video hiyo iliyowekwa katika ujumbe wa ilimuonyesha mfuasi wa Trump aliwa katika uwanja wa gofu huku akipaza sauti na kusema "nguvu ya wazungu ". Alionekana kuwa alikua akimjibu muandamanaji mwenzake aliyemuita mbaguzi wa rangi na kutumia maneno yasiyo ya staha. Waandamanaji wengine wanaompinga Trump walipaza sauti wakisema ''Nazi'' na maneno mengine ya shutuma dhidi ya waliohudhuria mkutano wa kampeni ya Trump.
Tim Scott, ambaye ndiye mtu mweusi pekee katika bunge la seneti la Marekani katika chama cha Republican, alisema katika mahojiano na CNN Jumapili kuwa video hiyo ilikua ni "kosa" na akamuomba rais aiondoe kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Bila shaka video ile isingepaswa kushirikishwa tena na anapaswa kuiondoa'' , Bwana Scott aliiambia televisheni hiyo.
Msemaji wa ikulu ya White House Judd Deere amesema kuwa rais "hakusikia kauli moja iliyotolewa katika video " lakini aliona "uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wengi wa wafuasi wake".
Waziri wa Afya na Huduma za binadamu wa Marekani , Alex Azar, aliiambia CNN kwamba " Awe rais , utawala wake au mimi mwenyewe ninaweza kufanya chochote kupata uungajimkono wa wazungu ".


EmoticonEmoticon