Tafiti Zimeonyesha Mtu Anaweza Kupata Corona Kupitia Vyoo Vya Kuflash

Choo cha Kuflash
Kusafisha au kusukuma maji ya choo cha ndani kunaweza kusababisha wingu ambalo linaweza kuvutwa kwa pua na kusambaza maambukizi, kama vile virusi vya corona, wanasema watafiti.

Wanasayansi wa China walibaini kuwa kuvuta maji yaani (kuflashi) choo kunaweza kusababisha mvuke unaoweza kupanda hadi nje ya bakuli la choo, na kufikia urefu wa mtu au hata zaidi.

Matone hayo yanaweza kuruka hadi umbali wa futi 3- au sentimita 91 - kutoka usawa wa bahari, kwa mujibu wa vipimo vilivyochukuliwa na kompyuta iliyotumiwa na wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha Yangzhou.

Kufunika choo wakati wa kusafisha kwa maji kunaweza kuepusha hili. Kazi hii ya wanasayansi imechapishwa katika jarida la fizikia ya vimiminika yaani Physics of Fluids.


EmoticonEmoticon