Tamasha La Muziki Coachella Lafutwa Kwa Mwaka Huu

Tamasha La Coachella
Tamasha la Coachella mwaka huu halitakuwepo tena kutokana na athari za ugonjwa wa virusi vya Corona ambazo zinaendelea. Limeripoti jarida la Billboard.

Jana Jumanne, Jarida hilo limesema kampuni ya Goldenvoice itapanga upya ratiba ya tukio hilo kutoka mwezi Oktoba mwaka huu ambapo ilipangwa kufanyika baada ya kuahirishwa mwezi April.

Hivyo huwenda Coachella ikafanyika April mwaka 2021, japo kampuni ya Goldenvoice inayoandaa tamasha hilo, haijaweka wazi taarifa rasmi.


EmoticonEmoticon