Tekashi 69 Amtolea Uvivu Cardi B

Baada ya kufanikiwa kuchumpa hadi nafasi ya kwanza Kwenye Billboard Hot 100, rapper Tekashi 6ix9ine amemuwashia moto female rapper Cardi B kwa madai ya kutuma watu wake kumtukana na kumdhihaki Kwenye mitandao ya kijamii kwa mafanikio ya ngoma yake wakidai kuwa ngoma hiyo 'Trollz' aliyofanya na Nick Minaj haistahili kukaa kwenye nafasi hiyo. 
Kupitia InstaStory Tekashi amewachana mashabiki hao wa Team 8 ikiwemo ya Cardi B ambao walikuwa wanapambana hadi kuchangisha fedha ili kuilipia ngoma ya DaBaby Rockstar ili iendelee kukaa number 1 on Billboard Hot 100 |


EmoticonEmoticon