Tekashi 69 Yupo Hatarini Mwanasheria Wake Athibitisha, Aweka Rekodi Mpya Billboard

Tekashi 69
Hali ya kiusalama ya Tekashi 69 ipo hatarini, mwanasheria wake azungumza. Akiwa amebakiza takribani miezi miwili ili amalize kifungo chake na awe huru, Tekashi 69 anaonekana kuwindwa na mtaa.

Mwanasheria wake Dawn Florio aliuambia mtandao wa New York Post jana (June 21) "Watu wengi walimshutumu Daniel [Tekashi 69] kwa kushirikiana na Serikali. Hata kijana mdogo wa kikundi cha uhalifu anayetaka kujitengenezea jina atajaribu kufanya kitu kwake." alieleza Dawn.

Pindi akimaliza kifungo chake cha ndani, 69 alipanga kuihama New York na kwenda kwenye mji ambao ni salama zaidi, na pia kuajiri 'bodyguard' kumuangalia. "Yupo kwenye imani kubwa sana lakini siwezi kupumzika hadi anahama na kupata sehemu nyingine yenye ulinzi masaa 24." aliongeza mwanasheria wake.

69 anayefanya vizuri na ngoma yake ya "Trollz" aliomshirikisha Nicki Minaj, umefanikiwa kukamata namba 1 kwenye chart hiyo kwa wiki hii na kuweka rekodi ya kuwa wimbo wake wa kwanza kuwahi kukalia nafasi hiyo.


EmoticonEmoticon